Quavo amjibu Chris Brown

Quavo amjibu Chris Brown

Baada ya mwanamuziki kutoka nchini #Marekani, Chris Brown kuachia listi ya ngoma alizoziongeza kwenye albumu yake ya '11:11’ huku ngoma yake ya ‘#Freaky’ ikitajwa kuwa ni dongo dhidi ya ‘rapa’ Quavo, hatimaye ‘rapa’ huyo amerudisha mashambulizi na kumjibu Chris.

Quavo siku ya jana ameachia ngoma mpya iitwayo ‘#Tender’ ambayo mashairi yake yanamtuhumu Chris Brown kuwa alikuwa akimdhalilisha mpenzi wake wa zamani na kumlazimisha kutumia madawa ya kulevya.

Wawili hao wapo katika bifu toka mwaka 2017 baada ya #Quavo kudaiwa kutoka kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wa #ChrisBrown Karrueche Tran.

Aidha si mara ya kwanza kwa wasanii wa hip-hop nchini humo kurushiana madongo, utakumbuka wiki kadhaa zilizopita Drake pamoja na Kendrick Lamar waliingia kwenye vichwa vya habari baada ya Lamar kumjibu Drake kupitia ngoma yake mpya.

Hata hivyo kupitia mabifu hayo siku kadhaa zilizopita Drake alidai kuwa muziki wa Hip-hop hautakuwa na amani kutokana na ushindani uliopo kwa baadhi ya mastaa ambao kila mmoja anataka kuonekana bora kuliko mwengine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags