Qayllah Shetta na ndoto ya kuwa Rais wa Tanzania

Qayllah Shetta na ndoto ya kuwa Rais wa Tanzania

Habiba Mohamed

Nyie nyie nyie ama kweli mtoto wa nyoka ni nyoka bwana weee kumekuwa na gumzo mitandaoni baada ya mtoto wa Shetta mwanae huyo anaefahamika kwa jina la Qayllah amefunguka na kusema kuwa yeye ndo Rais ajae.

Qayllah ni Binti wa miaka 9 mwenye ndoto ya kuwa rais wa Tanzania miaka ijayo, kupitia mahojiano Yake na chombo Cha habari maarufu afunguka machache kuhusiana na ndoto yake ya kuwa Rais wa Tanzania kwa miaka ijayo"Ndoto yangu ya kuwa Rais ilipata nguvu zaidi baada ya Mh. Samia Suluhu kuingia madarakani, nikaona kumbe wanawake tunaweza kupata nafasi kubwa ya uongozi na kufanya vizuri Toka hapo nikaanza kufatiria hotuba za Mh. Samia Suluhu Ili kujifunza zaidi" amesema Qayllah

Ifahamike kuwa Qayllah ni mtoto wa msanii kubwa wa mziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu "shetta" binti huyo alieleza pia Baba yake Shetta amempa support kubwa katika kupambania na kuishi katika ndoto hiyo ya kuwa Rais ajae.

vilevile katika kusapport harakati za Mh. Samia Suluhu ,Qayllah aigiza kama Mh. Samia Suluhu katika kuhamasisha zoezi zima la sensa inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 ,August 2022

Aidha shetta akiwa kweye moja ya mahojiano na chombo cha habari alisisitiza watu kujitokeza kuhesabiwa pia wazazi kuwasupport watoto kufikia ndoto zao kwani watoto wamebeba maono kwa ajiri ya Taifa la kesho.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags