Na Michael Anderson
Punguza marafiki ambao ukiwaambia unataka kufanya kitu wanakujibu "utawezaaa?" punguza marafiki ambao kutwa wanataka mchafue meza bar.
Punguza marafiki ambao umeongea nao kitu mkiwa wawili mwisho wa siku unakikuta kimeenea sehemu nyingine, punguza marafiki ambao wako right kila siku wenyewe hawataki kuambiwa wamekosea.! punguza marafiki ambao wakija kwako wao urafiki unahamia kwa mumeo au mkeo aliyekaa sebuleni wakati wewe kakuacha nje.!
Punguza marafiki ambao wanakuwa na urafiki na maadui zako kwa ukaribu zaidi. Punguza marafiki wa kwenye raha tu ukiwa na shida unajikuta peke yako. Punguza marafiki wanaokusifu huku wakijua umekosea.
Punguza marafiki ambao kila ukiwapigia simu na wao utawasikia yaani nilitaka kukupigia sasa hivi.!
PUNGUZA MIZIGO ISIYOKUWA NA UMUHIMU BAKI NA HAWA
Mtu atakayekulea kiroho , atakayekuongoza katika ndoto na maono yako mlezi wa familia yako pamoja na wazazi hawa ndio mtu muhimu sana kwenye safari yako usiwakose ili uweze kusonga mbele.
Sifa zao kabla hujawachagua ni za muhimu sana ili wasije wakakupoteza badala ya kukufikisha kule unakotaka kwenda.
Awe na mafanikio (amefika mbali) kwenye hiyo sehemu. Awe na tabia njema zinazokubalika na jamii yake na dini yake. (mfano hapa ukikutana na mtu ambaye anakuelekeza kuhusu biashara, mlevi na mzinzi hizi tabia lazima atakuambukiza kwa sababu atakua mtu wako wa karibu sana)
Awe amekuzidi sana kwenye kile unachotaka akulelee (akuongoze).
Watu utakao kutana nao chuoni muda wote
- Watu majani
- Watu tawi
- Watu mizizi
WATU MAJANI:
Hawa ni watu ambao wanakuja katika maisha yako kwa msimu tu. Huwezi kuwategemea kwa sababu ni dhaifu. Wanakuja kuchukua tu wanachotaka, lakini upepo ukija wataondoka. Unatakiwa kuwa makini na hawa watu maana wanakupenda mambo yakiwa sawa ila upepo ukija watakuacha.
WATU TAWI:
Wana nguvu, lakini unahitaji kuwa mwangalifu nao pia. Wanaachana wakati maisha yanakuwa magumu na hawawezi kuhimili uzito mwingi. Wanaweza kukaa na wewe katika baadhi ya misimu, lakini wataondoka hali inapokuwa ngumu zaidi.
WATU MIZIZI:
Watu hawa ni muhimu sana kwa sababu hawafanyi mambo ili waonekane. Wanakuunga mkono hata ukipitia wakati mgumu watakunywesha maji wakati wa kiu, watakulisha wakati wa njaa, na hawaguswi na msimamo wako wanakupenda hivyo hivyo. Siyo watu wote unaokutana nao ni marafiki zako, watabaki na wewe. Ni watu wa aina ya mizizi pekee ndio watakaa bila kujali msimu
Leave a Reply