Priyanka Chopra aeleza jinsi mama yake alivyomsaidia kuhifadhi mayai yake

Priyanka Chopra aeleza jinsi mama yake alivyomsaidia kuhifadhi mayai yake

Hellow! I hope uko pouwa mwanangu sana, sasa kama kawaida yetu simnajua kuwa hatunaga mba mba mba, basi bwana kwenye unique story leo tunakusogezea mwanadada ambae amefanya makubwa kwenye tasnia ya movie huko nchini India.

Priyanka Chopra mwenye umri wa miaka 40 kufuatia interview yake ya hivi karibuni ameeleza kuwa anamshukuru mama yake mzazi kwa kumshauri agandishe mayai yake ya uzazi yahifadhiwe kwasababu hakuwa tayari kuanzisha familia kwa wakati huo. 

Alieleza kuwa wamefanya hivyo kwasababu hata likitokea tatizo baadae kwenye mwili wake ambalo litampa shida kupata mtoto isiwe kikwazo sababu htayari mayai yake yalishahifadhiwa.

Ushauri huo aliufuata akiwa mwanzoni mwa miaka yake ya 30 kwasababu alitaka kufanikiwa kwanza katika kazi zake na kufikia malengo aliyojiwekea, hata hivyo wakati huo hakuwa amepata mume wa kueleweka ambae ataanzisha nae familia. 

Aliendelea kwa kuelezea kuwa hakutaka kuingia katika mahusiano na mume wake Nick Jonas mwenye umri wa miaka 30 kwa kudhania kuwa umri aliokuwa nao kipindi hicho asingependa kuitwa baba, ila mungu si athumani haikuchukua mud asana wakaoana.

Katika ndoa yao kulitokea misukosuko mingi na kwa bahati mbaya Priyanka alipotaka kupata mtoto ikawa sgida, hivyo basi ilibidi yeye na mumewe wakodishe tumbo la mwanamke mwingine awabebee mimba kupitia mayai ya Chopra yaliyohifadhiwa na kuyarutubisha kwa mbegu za Nick Jonas ambapo baadae walifanikiwa kupata mtoto wa kike kupitia mwanamama aliewabebea mimba.

Mwanadada huyo kupitia interview yake hiyo hiyo ameamua kuwashauri wanawake wenzie kama hawapo tayari kuzaa mapema basi wahifadhi mayai yao ya uzazi kama wana uwezo wa huduma hiyo, kuliko kuwekeza pesa katika kununua magari na vitu vya thamani.

Mama mzazi wa Priyanka  ambae ni producer wa filamu lakini pia ni daktari wa binadamu na taaluma yake imejikita zaidi kwenye mambo ya uzazi kwa wanawake na afya zao kwa ujumla

Ukiachilia mbali na muigizaji huyo mkongwe kutoka nchini India pia mwanamitindo maarufu, Kendall Jenner miezi ya karibuni alishauriwa na mama yake ayagandishe.mapema mayai yake yahifadhiwe baada ya kuonesha hayupo tayari kuzaa kwasasa

Ikumbukwe tu kisayansi wanawake kuanzia miaka ya 35 wengi hupata shida kubeba mimba, na biological clock ni moja wapo ya sababu kuu wanawake mbalimbali wenye uwezo kuamua kugandisha mapema mayai yao. 

Jambo la kushangaza ni kuwa Priyanka ana wanaweza kuongeza watoto wengi Zaidi wakiamua kupitia mayai yake yaliyohifadhiwa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags