Poshy Queen afunguka kuhusu ndoa yake iliyopita

Poshy Queen afunguka kuhusu ndoa yake iliyopita

Mrembo na mfanyabiashara Poshqueen amefunguka kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake aliyowahi kufunga mwaka 2020 na John ambaye ni raia wa Nigeria huku chanzo kikubwa kikitanjwa kuwa ni umbali kati ya wanandoa hao.

Posh amefunguka hayo wakati alipokuwa kwenye moja ya mahojiano yake Leo Agosti 16, 2024 huku akifunguka kiundani kuhusiana na sababu iliyomfanya aachane na ndoa yake hiyo.

“Niliolewa 2020, na nilikaa kwenye ndoa mwaka na nusu na ndoa yetu ilivunjika kutokana na utofauti wetu wa mila ambao ndio ulikuwa chanzo kikubwa cha kuachana lakini pia umbali kati yetu”

Mbali na hayo mrembo huyo alifunguka pia kuhusiana na ugomvi wake yeye na mpenzi wake wa sasa mwanamuziki Harmonize uliyotokea siku chache zilizopita.

“Mimi na Harmonize hatukugombana kisa kauli aliyotoa kuhusu wanawake wa Yanga lakini pia hatukugombana katika tafrija baada ya siku ya Yanga, ugomvi wetu niwamambo yakimahusiano na sichochote kile, lakini pia yanayosemwa sio yakweli” amesema Posh

Utakumbuka kuwa wawili hjao walianza mahusiano Januari 2024 ambapo mpaka kufikia sasa wametimiza miezi nane kwenye uhusiano huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags