Portable amtolea povu Davido

Portable amtolea povu Davido

Mwanamuziki wa Nigeria, #Portable, amemtolea povu mkali wa Afrobeat Davido kwa kudai kuwa msanii huyo alimtumia vibaya kwa ajili ya kutafuta umaarufu na kumuacha bila msaada wowote.

Portable ameyasema hayo kupitia video yake inayoendelea kusambaa mitandaoni akidai kuwa Davido alimuahidi kumpa mstari kwenye ngoma yake lakini hakufanya hivyo badala yake alimtumia kwa ajili ya ‘kutrend’.

Aidha msanii huyo alieleza jambo lililomuumiza zaidi ni baada ya kutumia First Class ya Ndege kusafiri kwenda Marekani kwa ajili ya nyimbo za Davido lakini mambo yalikuwa tofauti baada ya Davido kutomthamini.

Hata hivyo kwa sasa Davido amem-unfollow Portable kwenye Instagram baada Portable kumshutumu kwa kumpa ushauri mbaya kuhusu muziki wake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags