Polisi China kushughulika na wanaopaki magari vibaya

Polisi China kushughulika na wanaopaki magari vibaya

Polisi nchini #China wamezindua kifaa aina ya roboti ambacho kinauwezo wa kuhamisha magari yaliyoegeshwa vibaya.

Kifaa hicho ambacho kilipewa jina la ‘#Valet’ kinauwezo wa kuinua gari ambalo limeegeshwa vibaya na kuliweka sehemu nzuri, huku lengo la kuanzishwa kwa kifaa hicho ni kupunguza msongamano kwenye sehemu za maegesho.

Aidha kifaa hicho kilizua mtafaruku kupitia mitandao ya kijamii baada ya watu kuwa na mashaka huenda teknolojia hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia wezi kuwaibia magari yao kirahisi, lakini polisi nchini humo wameweka wazi kuwa kabla kifaa hicho akijaanza kuuzwa kwa kampuni basi watatafuta njia ya kuzuia suala hilo.

Hata hivyo kwa sasa vifaa hivyo vimeanza kufanya kazi katika viwanja vya ndege ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Charles du Gaulle karibu na #Paris.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags