Polisi kutoka nchini Iraq amekutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha kutokana na kifo cha mchambuzi mashuhuri wa masuala ya usalama na mkosoaji wa mara kwa mara wa wanamgambo wenye nguvu.
Hukumu hiyo iliyotolewa jana siku ya Jumapili, katika kipindi cha karibu miaka mitatu baada ya mchambuzi huyo kupigwa risasi nje ya nyumba yake Baghdad kufuatia vitisho vya wanamgambo.
Familia ya marehemu, Hisham al-Hashimi, imeonesha kufurahishwa na uamuzi huo lakini pia imeonesha wasiwasi kwamba uenda ikabatilishwa na kukatiwa rufaa.
Aidha Al-Hashimi aliyekuwa na umri wa miaka 47, aliuawa kwa kupigwa risasi Julai 2020 mbele ya nyumba yake huko Baghdad na washambuliaji wawili waliokuwa kwenye pikipiki baada ya kupewa vitisho kutoka wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran.
Chanzo DW
Leave a Reply