Poland yataka kulipwa fidia na Ujerumani kutokana na uharibifu uliotokea katika vita ya pili vya dunia

Poland yataka kulipwa fidia na Ujerumani kutokana na uharibifu uliotokea katika vita ya pili vya dunia

Serikali ya Poland inataka kuongeza shinikizo dhidi ya Ujerumani kuhusu suala la kulipwa fidia ya vita vya pili vya dunia. Kwa mujibu wa naibu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Arkadiusz Mularczk, Poland inataka kufikia lengo lake hilo kwa sababu ni muhimu kwa nchi hiyo na sio suala la kisiasa.

Naibu waziri huyo wa mambo ya nje wa Poland pia amesisitiza kwamba Ujerumani inaweza kuchagua ama kukaa kwenye meza ya mazungumzo au Poland italiibua suala hilo katika majukwaa yote ya kimataifa katika Umoja wa Mataifa, baraza la Ulaya na katika Umoja wa Ulaya.

Aidha Mularczyk ambaye pia ni mwenyekiti wa tume maalum ya bunge nchini Poland kuhusu suala hilo amesema kuna ripoti iliyoandaliwa kuhusu uharibifu uliofanywa dhidi ya Poland na utawala wa Wanazi wa wajerumani wakati wa vita vya pili vya dunia. Uharibifu huo unafikia dola Trilioni 1.3.

 

Chanzo DW






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post