Petitman Wakuache atarajia kufunga ndoa hivi karibuni

Petitman Wakuache atarajia kufunga ndoa hivi karibuni

Hellow! It’s another Monday mwanangu sana. Kama kawaida yetu tunakusogezea mastori mbalimbali, basi bwana leo tumekusogezea story ya mwanakaka Petitman Wakuache ambae amekuwa gumzo sana kupitia mitandao ya kijamii baada ya kumvalisha pete mpenzi wake ambae pia ni mzazi mwenzake anaefahamika kwa jina la Mama Kian.

Basi bwana wambea wakapeleleza unaambiwa pete hiyo imetajwa kuwa na thamani ya Tsh Million 3 za Kitanzania, ambapo sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa kede kede ikiwemo Hamisa Mobetto, Lulu Diva na yule mtaalam wa kuvaa, bwana Rich Mitindo na mastar wengine kibao.

Sasa bwana kumbe kijana yuko vizuri, unaambiwa mwamba Petitman akifunga ndoa hiyo basi itakuwa ndoa yake ya 3 ambapo moja wapo ya ndoa yake ni ile yeye na dada wa msanii mkubwa nchini Diamond, Esma Platnumz.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post