Did you know! in your life you must appreciate your self kwa uwezo mkubwa na kipaji kikubwa ulichonacho? Yeees!! Nagongelea msumari hapa lazima tukubali uwezo tulionao na tujivunie bhana acha kujidharau unaweza kuwa imara na kufika mbali zaidi kupitia kipaji chako au uwezo uliyobarikiwa.
Kutokujikubali na kutokuthamini kipaji na uwezo uliyokuwa nao ni Mwiko! Haifai leo namleta kwako kijana ambae amesimama na kipaji chake na kubadilisha historia ya maisha yake.
Hapa namleta kwako kijana Petit Afro ukiwa mpenzi wa dance basi jina hili halitokua geni kwako bila shaka vijana wengi tunamfahamu mnenguaji huyu kutokana na kazi zake anazo zifanya na hapa anasimulia mlolongo mzima wa kazi yake.
“ Mimi ni mmoja kati ya wanenguaji ambao wameanza kuweka machapisho yao YouTube barani Ulaya kupitia ngoma za Afrika hatukuwa wengi nilikuwa mimi na Sherrie Silver kutoka Rwanda”anasema na kuongeza kuwa.
“Tulipata watazamaji mwanzoni kabisa ilikuwa ukiingia youtube ukiandika Afro dansi zinakuja video zangu kwa sababu nilikuwa natumia watoto hivyo ilikuwa rahisi sana kufikisha habari kwa wenzao,”anasema.
Kauli hiyo ameitoa mnenguaji maarufu anaetambulika kwa jina la Petit Afro ambae anafanya shughuli zake hizo huko barani Ulaya anaefuatiliwa na watu wengi zaidi duniani.
Akizungumza na jarida la Mwananchi Scoop, Petit Afro ameweka wazi sababu ya video zake kupata watazamaji wengi zaidi ya milioni 50 duniani.
Akitoa majibu ya suala hilo Petit Afro ameeleza kuwa watu huangalia zaidi ya mara moja video zake kwa sababu hutumia kama darasa watu kujifunza namna ya kucheza style mbalimbali katika unenguaji.
“Mtu anaangalia video zaidi ya mara moja kutokana na kujifunza zile style, kwa sababu ni rahisi lazima mtu arudie kutazama na hiyo ndiyo sababu ya video zangu kufikisha watazamaji hao,”anasema.
Aidha Petit Afro ameweka wazi kuwa kutokana na kazi yake hiyo imemuongezea wanachama 1.7 milioni kwenye akaunti yake ya YouTube huku akiwa na zaidi ya video 200.
Namna alivyofanikiwa kufika ughaibuni
Petit Afro akiwa ni Mwafrika anayetokea hapa nyumbani nchini Tanzania ambaye alianza safari yake ya kwenda ughaibuni kupitia mama yake mzazi ambaye anaishi huko tangu mwaka 1990.
“Nimekwenda Ulaya kuishi sikwenda kudansi, wala kusoma, nilienda kwa mama yangu Uholanzi ambaye naye ni Mtanzania,”anasema.
Wakati akiwa anaishi huko kupitia agizo la Serikali alipata fursa ya kwenda kujifunza unenguaji hadi kufikia hatua ya kuwa mwalimu wa masuala hayo.
Hata hivyo amesema mnamo mwaka 2012 ndipo alipoanza rasmi kuwa mwalimu wa unenguaji huko barani Ulaya akiwa ameanza na watoto takribani 13 tu kwa kipindi hicho.
“Jinsi nilivyokuwa nikifundisha watoto walivutiwa sana na baada ya kupata likizo nilivyorudi kwa awamu nyingine watoto waliongezeka na kufikia 40," anasema.
Historia yake kwenye unenguaji
Aliwahi kushinda kwenye mashindano ya Azonto mnamo mwaka 2012 ya shindano la Afrikan dance kupitia tukio hilo ndipo alipopata nafasi ya kuwa mwalimu wa unenguaji huko ughaibuni.
Mnamo mwaka 2015 alipata fursa ya kushiriki pia katika mashindano ya Runinga nchini Uholanzi yaliyotambulika kwa jina la ‘every body can dance’ na kubahatika kuwa mwafrika wa kwanza kwenye shindano hilo.
Vile vile anaeleza kuwa kupitia mashindano mbalimbali ambayo alishiriki yalimuhamasisha kuendelea kufanya kazi zake kwa weledi mkubwa hadi kufikia hatua ya kutengeneza video zake na kuweka Instagram pamoja na YouTube.
“Rockonolo dance nilicheza na mwanafunzi wangu angle ambaye niko nae tangu akiwa na umri wa miaka saba hadi sasa ana miaka 12 Diamond aliiposti ile video na ikatusaidia pia kutusogeza mbele,”anasema.
Namna kazi yake inavyomuingizia kipato
Petit Afro amesema kuwa yeye ananufaika kupitia kazi yake ya ualimu wa unenguaji ambapo ana wanafunzi anaowafundisha hivyo anapata kipato kupitia kazi hiyo.
Hata hivyo ameongeza kuwa wakati mwengine yeye binafsi anakodisha ukumbi na kugharamia kila kitu wakati watu wanapokuja kuangalia maonyesho yake hapo ndipo anapowachaji kiasi cha pesa.
Vilevile ameweka wazi kuwa njia nyingine inayomuingizia kipato chake ni kuandaa Semina analipia matangazo, ukumbi na kila kitu baada ya hapo kitakachopatikana ndiyo cha kwake
“Mara nyingi pesa ninayoipata huwa naitumia kupelekea watoto yatima kwa hapa nyumbani huwa nafanya hivyo” anasema.
Soko la unenguaji Ulaya liko vipi?
“Kwa upande wa Ulaya watu kule wanaheshimu sana wanasapoti dansi hadi wazazi wanaisapoti pia katika kuitangaza kupitia watoto wao.”
Hata hivyo akielelezea namna anavyofanya kazi zake Petit Afro anasema kuwa yeye anashirikiana na mpigapicha wake ambaye pia ni mchezaji hivyo anatambua.
“Timu yangu ni watu wawili tu ikiongozwa na mimi mwenyewe ambaye ndiyo mkurugenzi pamoja na mpigapicha wangu ndiye anayefanya majukumu mbalimbali katika kazi zangu,”anasema.
Wasifu wake
Petit Afro ni kijana wa Kiafraka ambaye ni Mtanzania aliyekulia jijini Dar es Salaam mtaa wa Togo Kinondoni na kubahatika kuanza elimu yake ya Msingi katika shule ya Kinondoni, Tabata na Ikwiriri mkoa wa Pwani.
Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi alifanikiwa kujiunga na shule Sekondari Makongo High School na kumalizia elimu yake ya kidato cha nne Shuleni hapo.
Kisha kutimkia Ughaibuni na kuweza kufanya makubwa zaidi kupitia uwezo wake na kipaji alicho nacho huyo ndiyo kijana Petit Afro.
Eebwanaa usiogope mtu wangu kila mishe ni mishe tu iheshimu, ithamini kwani heshima ya mishe yako inaanzia kwako! Pambana piga kazi usichokeee happy furahiii day!!!.
Leave a Reply