Padri afukuzwa baada ya kugundulika ana mtoto

Padri afukuzwa baada ya kugundulika ana mtoto

Kiongozi Mkuu wa Kanisa la katoliki nchini Ufaransa Papa Francis amechukua uamuzi wa kumtimua Padri Wenceslas Munyeshyaka mzaliwa wa Rwanda ambaye alikuwa akitumikia kanisa hilo nchini humo takribani miaka 30.

Ofisi ya Dayosisi ya Évreux imesema Papa alisaini amri ya kuondolewa kazini kwa mtumishi huyo tangu machi 2023 baada ya kuthibitisha Munyeshyaka aliyekimbia mauaji ya Kimbari Mwaka 1994 ana mtoto wa kiume mwenye miaka 10

Aidha Munyeshyaka aliteuliwa kuwa kasisi nchini Rwanda mwaka wa 1992 ambako pia alituhumiwa kuhusika na mauaji ya mamia ya Watutsi waliokimbilia kanisani kwake huko mji Mkuu wa Kigali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags