Pablo: Azungumzia ushindi dhidi ya Orlando

Pablo: Azungumzia ushindi dhidi ya Orlando

Kocha mkuu wa Klabu ya Simba  Pablo Franco, ameweka wazi furaha yake ya ushindi wa bao moja nyumbani waliopata dhidi Orlando Pirates akisema unampa faida kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo nchini Afrika Kusini.

Pablo amesema michuano ya Afrika ni migumu hivyo unapaswa kutumia vema uwanja wa nyumbani ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye mchezo wa marudiano.

Pablo ameongeza kuwa wanatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Orlando kwenye mchezo wa marudiano lakini wamejipanga kuhakikisha wanaenda kufanya vizuri ugenini.

Pablo amekiri kuwa hawakuwa na matokeo mazuri kwenye mechi za ugenini katika hatua ya makundi kwa hiyo wanapaswa kujipanga hasa kutokana na ubora wa wapinzani.

“Michuano ya Afrika mara nyingi timu zinafanya vizuri nyumbani kama tulivyofanya. Tutajipanga kuelekea mchezo wa marudiano ugenini tunahitaji kufuzu nusu fainali,” amesema Pablo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags