P Funk  Amkataa Kajala

P Funk Amkataa Kajala

Kutoka kwa Producer wa muziki wa Bongofleva, P Funk ‘Majani’ amesema kwa sasa hahitaji kuzungumza na mzazi mwenzake, Kajala Masanja kwani amekuwa akimshauri mambo mengi kuhusu mtoto wao, Paula lakini anayapuuzia.

Majani ameyasema hayo hivi karibuni wakati akifanyiwa mahojiano na vyombo vya habari huku akisema kuwa kwa sasa Paula amekua na wanaongea vizuri, hivyo hana haja ya kuongea na Kajala badala yake atazungumza na Paula moja kwa moja kama kuna jambo la kumshauri.

P Funk amedai kuwa Kajala amekuwa ni mtu wa drama na ameshindwa kubadilisha tabia, lakini kwa vile mwanaye sasa anajitambua, yeye ataendelea kumpa ushauri mwanaye.


“Mama is toxic mimi na yeye hatuelewani, mimi niko kwenye ndoa na mwanamke kwa miaka 12 na amenizalia watoto watatu, kama mtu ana drama una-avoid kidogo. Sababu unapotoa ushauri, unamwambia hiki kitakuja kukugeukia, yeye hajali.

“Paula bado ni mdogo, ana nafasi ya kubadilika tabia, lakini mama yake yule ‘let it be’ kwa kweli sisi hatuongei, sihitaji kuongea naye tena, sababu Paula ana umri tayari ambao ni mtu mzima. Kama kuna salam tutasalimiana, kama tutaonana sehemu tutasalimiana,” amesema P Funk.

Kama kawaida mdau unaweza kudondosha comment yako hapo chini kupitia ukurasa wetu wa www.mwananchi scoop.co.tz.






Comments 2


  • Awesome Image

    Ongea na mwana tu, mama yake kapuka tabia yake imekuwa kama ngozo yake

  • Awesome Image

    Ongea na mwana tu, mama yake kapuka tabia yake imekuwa kama ngozo yake

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags