Baada ya Mfululizo wa msimu wa pili wa Squid Game kufanya vizuri mara tu baada ya kuachiwa, wasambazaji wakuu wa filamu hiyo Netflix wametangaza ujio wa Msimu wa 3 utakaotoka mwaka 2025.
Kupitia ukurasa wao wa instagram wa Netflix wameweka chapisho la promo ya Filamu hiyo huku wakionesha rekodi ya filamu hiyo ambayo imeweka tangu kuachiwa kwake.
"Squid Game Msimu wa 2 ni onyesho 1 kwenye Netflix katika nchi 92 na tayari ipo namba saba kwa vipindi vya TV ndani ya Netflix maarufu na sio ya Kiingereza kitu ambcho akijawa kutokea! Sasa nani yuko tayari kwa Msimu wa 3 ?,” Wameandika Netflix kupitia ukurasa wao wa instagram.
Squid Game msimu wa pili iliachiwa rasmi Desemba 26, 2024 huku ikichezwa na mastaa mbalimbali wakiwemo Lee Jung-jae, Lee Byung-hun, Wi Ha-jun, Gong Yoo na wengineo.
Leave a Reply