P Diddy atimiza ahadi ya kuchangia dola milion 1

P Diddy atimiza ahadi ya kuchangia dola milion 1

Baada ya ‘rapa’ #PDiddy kutangaza katika Tuzo za #BET za 2022 kuwa atatoa dola milioni 1katika Chuo Kikuu cha #Howard, hatimaye ametimiza ahadi hiyo ambapo alikabidhi ‘cheki’ ya pesa kwa rais wa chuo Dk. Ben Vinson III.

#PDiddy alitoa pesa hiyo wakati wa tamasha chuoni hapo huku katika hotuba aliyoitoa akiwataka wanafunzi kushikamana na kudumisha urithi wa watu wenye ngozi nyeusi.

Licha ya kutoa msaada huo #Diddy aliwaburudisha wanafunzi wa chuo hicho cha watu weusi kwa kutumbuiza baadhi ya ngoma zake ikiwemo ‘I need a girl’.

P Diddy ameonekana katika filamu mbali mbali ikiwemo ‘A raisin in the sun’, ‘Get him to the greek’nk.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags