Osimhen aonesha jeuri uwanjani, Awajibu Napoli

Osimhen aonesha jeuri uwanjani, Awajibu Napoli

Baada ya mchezaji Victor Osimhen hivi karibuni kudai amedhihakiwa kupitia ‘akaunti’ ya TikTok ya ‘timu’ ya #Napoli,  sasa ‘straika’ huyo wa #Nigeria  amewajibu kwa vitendo jana katika ‘mechi’ dhidi ya Udinese iliyomalizika kwa ushindi wa 4-1.

Osimhen alifunga bao dakika ya 39 kwenye mchezo dhidi ya Udinesse akikamilisha bao la pili katika dakika hizo, ambapo dakika ya 19 mchezaji #PiotrZielisk alitia nyavuni bao la kwanza katika ‘timu’ hiyo.

Ingawa ‘staa’ huyo alionekana kukwazika baada ya kitendo cha kudhihakiwa na katika moja video zilizosambaa mtandaoni zilimuonyesha akikataa hata kupeana mkono na wachezaji wenzake alipowasili mazoezini kabla ya ‘mechi’ hiyo.

Ikumbukwe kuwa Osimhen alikumbana na dhihaka hizo baada ya kusambaa kwa video iliyokuwa inamuonesha akiomba ‘penati’ na kukosa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags