Nyota wa Hannah Montana aswekwa ndani, Adaiwa  kuiba chipsi

Nyota wa Hannah Montana aswekwa ndani, Adaiwa kuiba chipsi

Nyota wa zamani wa 'Hannah Montana',  Mitchel Musso  ambaye alicheza "Oliver Oken" akamatwa Texas kwa tuhuma zinazohusiana na wizi wa mfuko wa chipsi akiwa amelewa. Nyota huyo wa zamani wa Disney alikamatwa baada ya ‘polisi’ kuitwa na wahudumu wa ‘hoteli’ aliyokuwepo.

Baada ya ‘polisi’ kufika mashahidi walidai kuwa walimwona akichukua mfuko wa chipsi na kuanza kula bila kulipa na alipotakiwa kilipa alianza kutoa matusi.

Hata hivyo muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 32 baadaye alianzisha ugomvi hadi pale ‘polisi’ walifika na kugundua kuwa alikuwa amelewa.

Polisi walipofanya ukaguzi waligundua kuwa alikuwa na makosa mengine kama vile kutembea na ‘leseni’ ya udereva iliyoisha, wizi, ulevi

na kupelekea atiwe ndani hadi atakapotoa dhamana ya dola 1,000 ambayo ni zaidi ya tsh 2 milioni.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags