Nyota wa filamu ya Lucky afariki dunia

Nyota wa filamu ya Lucky afariki dunia

Mwigizaji wa Marekani James Darren, aliyetambulika zaidi kupitia filamu ya ‘Gidget’ afariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na mtoto wake Jim Moret akieleza kuwa baba yake amefariki siku ya jana Jumatatu Septemba 2, 2024 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Cedars-Sinai iliyopo Los Angeles.

Hata hivyo mtoto wa mwigizaji huyo Jim ameeleza kuwa baba yake alikuwa na matatizo ya moyo na alikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kubadilishwa Valve ya Aorta lakini alionekana kutokuwa sawa hivyo akapewa kitanda.

Licha ya kuonekana katika filamu mbalimbali pia amewahi kutoa ngoma kadhaa huku wimbo wake wa ‘Goodbye Cruel World’ ukishika nafasi ya 3 kwenye chati za Billboard mwaka 1961.

James Darren ameonekana kwenye filamu kama ‘Lucky’, ‘Aliens from Another Planet’, ‘Gidget’ , ‘Gunman's Walk’, ‘Operation Mad Ball’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags