Nyota wa ‘Beverly Hills’ aitamani talaka

Nyota wa ‘Beverly Hills’ aitamani talaka

Muigizaji kutoka nchini Marekani Kyle Richard anadai kuwa kutengana na mume wake kutawaathiri watoto wake kwa kiasi kikubwa ingawa itamfanya yeye kuwa na nguvu mpya.

Kwa mujibu wa TMZ News inaeleza kuwa msanii huyo amekiri amepitia mengi kipindi ambacho walitengana kwa muda mfupi na mume wake anayefahamika kwa jina la Mauricio, huku pia akieleza jinsi alivyo kuwa ngumu kukabiliana na familia akiwa pekeyake.

Kyle anasema bado wazo lake la talaka lipo akilini mwake mpaka sasa ataendelea kusisitiza uamuzi wake lakini inakuwa ngumu hasa akiwaona watoto wake watakuwa na maisha magumu bila baba yao.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 54 ameonekana kwenye filamu ya ‘The Real Housewives of Beverly Hills’ iliotoka mwaka huu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags