Njia za kupata marafiki baada ya kumaliza chuo

Njia za kupata marafiki baada ya kumaliza chuo

Hellow! Niaje niaje wanangu wa Mwananchi Scoop, I hope mko powa watu wetu wa nguvu, kama kawaida yetu katika segment yetu ya Unicorner leo tumekusogezea mada konki kabisa ambayo ukiisoma ukaielewa basi itakusaidia sana katika maisha yako.

Hapa tunazungumzia yale Maconnection ya marafiki wa muhimu sio wale wa kumaliza bar leo kidimbwi kesho kwenye visinia hapana, yaani hapa tunakupa nondo na njia za kupata marafiki ukishamaliza chuo ambao watakusaidia wewe kupata kazi au kupata uelewa hata wa kuanzisha biashara.

Kama tunavyojua wengi wetu tukishamaliza chuo kila mtu anafanya mambo yake yaani hakuna urafiki kama ule mliokuwa nao chuo kila mtu atakuwa anahangaikia maisha yake, waliokuwepo chuo sahivi hawawezi kunielewa kwasababu wanaona kila siku wapo chuo na marafiki zao na wanaamini kuwa hawata tengana lakini kwa waliokuwa mitaani wanaelewa situation nzima.

Kwa baadhi ya watu wanaweza kujiuliza kuwa kupata marafiki chuoni kunaweza kuwa rahisi lakini mtu anawezaje kupata marafiki baada ya chuo kikuu?

Kulingana na tafiti za hivi karibuni kuwa na marafiki wazuri kuna faida kwa afya yako ya akili na matamanio yako ya kimaendeleo Hata hivyo ikiwa umehitimu chuo kikuu hivi majuzi, kuhamishwa hadi eneo jipya, au vinginevyo umepitia mabadiliko makubwa ya maisha, kuna uwezekano mkubwa wa kutambua kwamba mzunguko wako wa kijamii unapungua.

Zaidi zaidi kukutana na watu wapya chuoni ni rahisi, lakini mara tu unapohitimu na kuacha jumuiya ya chuo, maisha yanaweza kuwa mengi zaidi peke yako yaani kila kitu unafanya peke yako sio kama zamani ulipokuwa chuoni unashare everthing na marafiki zako.

Kuna uwezekano mkubwa wa kuzungukwa na watu wa rika lako wanaopenda mambo yanayokuvutia kwa vile sasa uko ulimwenguni. Kwa hivyo kupata marafiki wapya wazuri kutahitaji kujaribu mbinu mpya na kunaihitaji kujitoa wewe mwenyewe kuanza kujitambua na kuachana na akili za kitoto.

Je kwanini ni ngumu kupata marafiki baada ya chuo?

Urafiki wa kweli ni ngumu zaidi kuunda kuliko ule ulioanzishwa chuoni. Malengo ya watu wengi hubadilika mara tu wanapohitimu chuo na kuhamisha mawazo yao kutoka kwa shughuli za kitaaluma hadi kwa shughuli za "watu wazima" kama vile kupata kazi na kuanzisha familia na kutunza wazazi wake.

Kupata marafiki wapya baada ya chuo kikuu inaweza kuwa uzoefu mgumu na wa kutisha Ingawa lengo lako kuu linaweza lisiwe kupata marafiki.

Siku hizi watu wanaangalia mtu wa kufanya nae maisha yaani kuenda nae katika mafanikio watu siku hizi wanabagua watu, ukijiuliza kwanini ni ngumu kupata marafiki baada ya kumaliza chuo kwasababu siku hizi baadhi yao wanaangalia yule mtu ambae yuko tayari kujitoa kwa jambo lolote lile na asiwe na akili za kitoto zile za chuoni.

Ni ngumu kupata marafiki kama bado unaakili za kitoto, au haujajielewa bado na haukuwa vizuri darasani hakuna atakaekubali kuongozana nawewe katika mafanikio kwasababu usipofanya bidii baada ya kuhitimu, hutakuwa na fursa nyingi za kuingiliana na watu wenye nia moja nje ya kazi na mafanikio.

Haya hizi ndizo baadhi ya kupata marafiki baada ya kumaliza chuo… 

  • Kujitolea

Hatua ya msingi ya kupata marafiki wapya baada ya kumaliza chuo ni Kujitolea. Kujitolea ni fursa nzuri ya kukutana na marafiki baada ya chuo na watakuwa bora kuliko wale uliotoka nao huko kwasababu wao akili zao zitakuwa zimepevuka kimaendeleo.

Kujitolea na watu wengine wanaoshiriki maslahi yako ni njia nzuri ya kukutana na watu wapya. Matukio ya kusafisha bustani, kusafisha pembezoni mwa bahari nk. Hizi ndizo sehemu utakutana na watu wakubwa na tofauti tofauti

Uundaji wa majopo ya ushauri wa raia ili kutoa maoni kuhusu masuala mbalimbali kama vile bustani na mipango ya jamii umeenea sana katika maeneo mbalimbali, hii itakusaidia san asana kwababu mishemishe hizi zinahusisha baadhi ya watu serikalini so itakupatia urahisi kukutana na watu wakubwa Zaidi.

  • Kudhuria matukio( Events)

Hatua nyingine nzuri ya kupata marafiki baada ya kumaliza chuo ni kuhudhuria shughuli na matukio mbalimbali, siku hizi bwana kuna event nyingi za vijana Mfano YADA nk matukio kama haya yanakukutanisha na watu wa mataifa mbalimbali, nazungumza hivi kwasababu nishawahi kuhudhuria event zao mara kadhaa. Itakusaidia kujifunza mambo mengi na ukitoka katika event yao moja basi wewe sio yule tunaekufahamu lazima utakuwa wa tofauti.

Ni rahisi kupata marafiki wapya kwenye mikusanyiko hii kwa sababu una angalau jambo moja linalofanana na wahudhuriaji wengine, hivyo iwe rahisi kuanzisha mazungumzo waswahili wanasema shobo, inabidi wewe ndo uanzishe maongezi na watu uliowakuta sio wao ndo wakuanze ikiwezekana badilishaneni namba kabisa.

Unachotakiwa kukifanya ni kuondokana na aibu, binadamu tumeumbwa na aibu na haya chakufanya nikuziachilia mbali kwasababu sasahivi uko kwa ajili ya kuanzisha maisha yako mapya na marafiki wapya, kwenye event mfuate mtu salimiana nae na badilishaneni namba hata kama sio kiongozi one day anaweza kuja kukusaidia kwa namna yoyote ile, pia usizarau watu kwa kuona yule hajavaa vizuri au hana muonekano mzuri ukaacha kumfuata utakuja kujuta baadae. 

  • Kuwa karibu na wafanyakazi wenzako

kwa wale ambao mmebahatika kupata kazi pindi tuu ulipo maliza chuo kuna jambo moja nataka kukueleza kuwa, sehemu ulipo either mahali pakazi chuo hata nyumbani sio sehemu ambayo utaiishi maisha yako yote, nikiwa namaanisha kuwa kama ni chuo utamaliza, nyumbani utaoa au kuolewa na kazini unaweza kufukuzwa pia.

Kuwa marafiki na watu unaofanya nao kazi, iwe umekuwepo kwa miaka kadhaa au ni mgeni kwa kampuni, inaweza kuwa kazi ngumu. Ukosefu wa ujuzi wa kijamii au uundaji wa vikundi vinaweza kukufanya uhisi kama mgeni katika mazingira mapya.

Ili kuepuka hili, jaribu kuzungumza kuhusu mada ambazo unafurahia na zinazokuletea furaha. Zaidi ya hayo, zuia porojo za ofisi wakati wewe na wenzako mnapokutana. Jaribu kuangalia na marafiki maana kazini kila rafiki ana nia yake kwako so cha kuzingatia ni kuwa makini.

Katika maisha haya hakuna mtu anataka kuwa rafiki yako ikiwa anashuku kuwa wewe sio mwaminifu. Badala ya kushindana na wafanyakazi wenzako kupanda ngazi ya ushirika, shirikianeni kusukumana vyeo na sio kuoneana wivu.

Itaendelea…






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post