Njia za kumwambia bosi wako una tatizo na mfanyakazi mwingine

Njia za kumwambia bosi wako una tatizo na mfanyakazi mwingine

Niaje mwanetu!! I hope uko byee na haka ka weekend kaliko changenyika na sikukuu basi mpaka raha lakini tupo kukujuza kila kitu hata ambacho ulikuwa unakisikia basi sisi tuna kuwekea bayana mwanetu sana.

katika segment ya kazi bana wiki ilio pita tuliweka mada ya njia nzuri za kupongezana kazini, kama bado hujasoma fanya kutembelea website zetu ili uweze kujua Zaidi tulichokieleza.

Leo tunakusogezea jinsi ya kumwambia bosi wako una tatizo na mfanya kazi mwenzio wengine, unaweza kusema kama ni kaumbea furani hivi kumshtakia bosi wako maudhi ya mfanyakazi mwenzio la hasha sometimes ina kuwa too much lazima ufikeshe ngazi za juu ili upate solution na ufanye kazi kwa amani.

Katika mazingira bora ya kazi, mabosi na wafanyikazi huelewana kwa usawa, na wafanyakazi wenzao  huisi kama washiriki wanaoheshimika ni wa timu moja wakati mfanyakazi mmoja anasababisha matatizo kwa mwingine hata hivyo inaweza kufanya kazi kuwa ugumu.

Wafanyakazi wengine huwanyanyasa wengine, hukejeli mawazo ya wafanyakazi wengine au kushindwa kufanya sehemu yao ya kazi kwenye mradi ikiwa mfanyakazi mwenzako hana adabu, mvivu, ana tabia mbaya au maudhi tu,

Unaweza kufanya afukuzwe kazi kutoka na maudhi anayo yafanya kwa ujumla njia bora ya kufanyia kazi suluhisho hilo ikiwa hiyo haifanyi kazi, huenda ukahitaji kumwambia bosi wako kuhusu suala hilo.

  • Hatua ya kwanza

Andika tabia inayowasumbua wafanyakazi mwenzako kama hivi mfano ikiwa unahisi kuwa mfanyakazi mwenzako anakunyanyasa kwa kuongea utani wa kuudhi unapotaka kumfikishia ujumbe bosi wenu unapaswa kuandika tarehe ya tukio na kile hasa kilichotokea na ushahidi yaweza ikawa wanafunzi wenzio au laah.

  • Hatua ya pili

Una paswa kuzungumza na mfanyakazi huyo kuhusu matendo yake kwa faragha na kwa wakati unaofaa yaani kama onyo waweza fanya hivo wakati wa mapumziko ya mchana au baada ya kazi.

Eleza kwamba tabia yake inakufanya ukose raha au kupatwa na hasira mwambie abadilike na apendekeze njia ambazo anaweza kujiboresha yaani njia sahihi za utani, kuna baadhi yao utani wao hadi kwenye famililia.

Ikiwa atakataa jizuie kumfanyia ugomvi wowote ule kama kumpiga kichwani na badala yake mjulishe kwamba unaweza kupeleka suala hilo kwa bosi wako.

  • Hatua ya tatu

Tambua unachotaka bosi wako afanye kuhusu tatizo hilo kwa mfano ikiwa mfanyakazi anakunyanyasa bosi wako anaweza kukuuliza ikiwa unataka kushtaki kwa vyombo vya sheria au uhamie tu idara tofauti ili uweze kuepuka mfanyakazi.

  • Hatua ya nne

Tulia kabla ya kuzungumza na bosi wako usikimbilie ofisini kwake mara baada ya tukio lisilopendeza na mfanyakazi mwenzako hasira yako na kufadhaika kutafanya iwe vigumu kwako kuzungumzia tatizo hilo kwa uwazi.

Bosi wako pia anaweza asikuchukulie kwa uzito ikiwa unaropoka na kusema kama umerukwa na akili.

  • Hatua ya tano

Panga time ya kuzungumza na bosi wako wakati wa utulivu kama vile baada ya zamu yako au mwishoni mwa siku biashara inapofungwa jioni. wasiliana na bosi wako anapokuwa peke yake.

Hakikisha hana kazi kwa muda huo ili aweze kukupa umakini wake kamili, ikiwa hili haliwezekani, huenda ukahitaji kuweka miadi na bosi wako. hii inakupa muda uliowekwa wa kuzungumza juu ya suala hilo.

  • Hatua ya sita

Eleza tatizo ulilonalo kwa bosi wako wasilisha madokezo uliyoandika kuhusu tabia ya mfanyakazi mwenzako na toa ushahidi mwingine wowote ulio nao ongea kwa utulivu juu ya ukweli wa hali hiyo na ueleze wazi jinsi mfanyakazi huyo anavyoathiri kazi yako.

Ingawa inaweza kukufanya ukajisikia vizuri kwa kutoa dukuduku lako kuhusu mfanyakazi mwenzako anayekuudhi jizuie kushambulia utu wake au kuita jina lake.

  • Hatua ya saba

Sikiliza suluhu la bosi wako kwa tatizo yaani sikiliza bosi wako ata sema nini ikiwa hukubaliani na suluhu alio toa bosi wako jaribu wasilisha mawazo yako mwenyewe na uulize kama atayazingatia.

Kwa mfano, ikiwa bosi wako anasema atamfuta kazi mfanyakazi mwenzako anayekusumbua, lakini hufikirii kuwa adhabu kali kama hiyo ni muhimu, muulize kama atampa onyo tu.

Siku zote waswahili husema mficha maradhi basi kifo humuumbua sasa kabla haya yote hayajatokea matatizo makubwa sehemu ya kazi yako hakikisha una wasilisha changamoto zako sehemu husika kwa bosi wako au kwa meneja muajiri ili aweza kulitafutia solution mapema.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags