Njia bora za kufanikiwa kimasomo

Njia bora za kufanikiwa kimasomo

 

Na Janeth Jovin

Je umekua ukisoma sana nyakati za karibia na mitihani na bado matokeo ni finyu ukiringanisha na wakati unaotumia, bila kusahau kukesha usiku kucha? Soma zaidi upate siri ya kufanikiwa katika masomo yako katika ngazi tofauti tofauti za elimu ikiwemo elimu ya chuo kikuu.

Namna yakufanikiwa katika mchakato wakusoma:

KUWA NA FIKRA CHANYA:

Watu wengi uchukulia kusoma ni kama adhabu ambayo wamepewa na inawalazimu kusoma kwakua hawana njia nyingine ambayo wangeweza kufikia ndoto zao.

Kwa hali hii wengi husoma kwa lengo tu la kufaulu mitihani na wakishafaulu walichojifunza uishia kwenye mtihani. Kwa hali kama hii wengi wao uona ni heri wasome siku moja au usiku mmoja kuamkia kwenye mtihani.

Katika zama hizi hata zile za zamani mtu yeyote ambaye alikua anasoma kwa lengo la kufaulu mtihani basi mtu huyu yuko kwenye hatari kubwa sana.

Tumeshuhudia sikuhizi watu wengi wanamaliza vyuo vikuu wakiwa hawajui vema kazi zao na hii hutokana na wengi kutokujua nini haswa walichokua wanajifunza.

Hili limekua tatizo hata wanapoenda kuomba kazi na mabosi wao kuwaona hawana ujuzi wakutosha kuweza kuaminiwa katika kupewa kazi wanazoziomba.

Inampasa kila mtu ambaye ameamua kusoma ajue kwa undani anachosomea na aweze kukielezea na kukitenda kwa ufasaha, wepesi wa kufanya haya utakuja endapo kila mmoja atapenda kile anachojifunza na kuweka bidii kukijua kwa undani.

Faida iliopo ni kuwa hata kama mtu huyu hataajiliwa basi itakua rahisi kwake kubuni njia za kujiajili na kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira mtaani.

USIPENDE KUHARISHA MAMBO:

Kwa lugha ya kingereza tabia hii huitwa "procrastination", hili ni tatizo ambalo wengi wetu tunalo hasa kwa kazi ambazo zinaonekana kutohitajika hivi karibuni.

Mtu ujikuta anasogeza ratiba mbele ili aweze kuapata mda wakufanya mambo mengine ambayo andhani kua ni ya muhimu kuliko yalioko mbele yake.

Wanafunzi wengi katika ngazi mbali mbali hupoteza mda mwingi wakipiga soga na marafiki au wakicheza michezo ya video (video games), wengine huenda kwenye mambo yaoya biashara au hata kuzurula wakiamini kua watasoma dakika ya mwisho mtihaniukikaribia madhara ya kuhairisha mambo ni mengi ikiwemo

TAFUTA ENEO LA KIMYA:

Watu wengi usoma popote bila kujali kama eneo hilo linafaa kwaajili ya kusoma masomo binafsi, wakati wa kusoma ni vema ukatafuta eneo ambalo liko kimya na mbali na usumbufu wa namna yoyote kama marafiki wenye kupenda kupiga soga kila wakati au makelele ya magari na muziki.

Pia epuka kusikiliza muziki wakati ukiwa eneo la kusoma na nyingine nyingi. inaweza kuwa ni maktaba, chumba au eneo lakujificha cha msingi kue kimya,kuna mwanga wakutosha  na kuna hewa yakutosha.

Pasi kusahau watu wengi upenda kusoma wakiwa wanasikiliza mziki lakini hii huondoa mawazo yao kutoka kwenye umakini na badala yake huanza kusikiliza ala za muziki au mashahiri ya nyimbo wanazozisikiliza ni vema ukakwepa kusikiliza mziki wakati wakusoma hii itakusahidia kuongeza umakini wako kwenye jambo unalosoma.

TENGA MDA MAALUMU:

Chagua wakati au saa maalumu kwaajili ya masomo binafsi na mijadala ya makundi maarufu kama group discussions, chagua siku maalumu kwaajili ya masomo binafsi na mijadala ya makundi (personal studies and group discussions).

Tengeneza ratiba na ifuate kwa nidhamu kuu,pamoja na kua na ratiba lakini isikufanye ukose wakati wa mapumziko na kuchangamana na  watu wengine kama ndugu jamaa na marafiki. Hii itakusaidia kuupa nafasi ubongo wako kupumua na kuweza kutunza kumbukumbu vizuri.

KUWA NA VIFAA VYOTE KWAAJILI YA KUJISOMEA:

Vifaa vyako vyote utakavyo vihitaji hakikisha unavyo

Hakikisha unavyovifaa vyote utakavyohitaji wakati wakusoma vifaha hivo ni kama vitabu utakavovisoma,kalamu ya wino,kalamu ya risasi, rula, kifutio daftari yakuandikia point ulizojifunza.

kama unasoma mtandaoni kwa kupitia tarakilishi mpakato (laptop) basi hakikisha unajizuia kutumia tovuti zisizohusika kwenye mchakato wako wakusoma, unaweza kutumia program za kuzuia kwa muda utembezi (browsing) wa tovuti zisizohitajika kama kila wakati unapata ushawishi wa kusomaGoogle Chome facebook notification   unaweza kuweka program hii kwenye tarakilishi yako kuongeza umakini na uzuri ni kua itazuia vitembezi vyote kuruhusu utembezi wa tovuti ulizoziuia...

Pia zima simu yako ya mkono au iweke kwenye silent mode kuzia usumbufu wowote unaoweza kujitokeza itakua vizuri kama utaiweka sehemu usio weza kuiona kama kwenye begi mpaka utakapo maliza kusoma.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags