Night club ya Jay-Z yapigwa kufuli

Night club ya Jay-Z yapigwa kufuli

Night club inayomilikiwa na ‘rapa’ kutoka nchini Marekani Jay-Z ya 40/40 imefungwa baada ya miaka 20 na inatarajiwa kufunguliwa tena katika eneo jipya mwaka 2024.

Kwa mujibu wa Eater new York news imeeleza kuwa club hiyo iliyoko Manhattan, Falatiron imeacha kuendesha shughuli zake zote tangu mwisho wa mwezi Julai na wamepanga kuifungua tena katika eneo lingine mwaka ujao.

Club ya 40/40 ilifunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2003, ilijulikana zaidi kutokana na kufanyika sherehe za uzinduzi wa ‘albam’ na siku za kuzaliwa za watu mashuhuri, Jay-Z pia alifungua ‘hoteli’ za kupumzika huko Las Vegas, Atlantic City, Atlanta na katika Kituo cha Barclays cha Brooklyn.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags