Nigeria kuchunguza tambi zinazo sababisha saratani

Nigeria kuchunguza tambi zinazo sababisha saratani

Wakala wa kudhibiti Chakula na Dawa (Nafdac) nchini Nigeria imesema inachukua hatua za haraka kuchunguza aina maarufu ya tambi za Indomie baada ya madai ya kuwepo kwa 'substance' ya Ethylene Oxide inayohusishwa na kusababisha Saratani.

Ethlene Oxide ni gesi isiyo na rangi inayoweza kuwaka moto Inayotumiwa hasa kuzalisha Kemikali nyingine, huweza kutumiwa kama Dawa ya kuua wadudu na kutakasa vifaa vya kitabibu.

Aidha Nafdac ilisema uchunguzi huo unafuatia zuio la hivi karibuni la kuuzwa kwa tambi zenye ladha ya Kuku Nchini Malaysia  na  Taiwan baada ya 'substance' hizo kugunduliwa katika sampuli 11 kati ya 36 za kampuni mbalimbali. 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags