Tasnia ya muziki wa Bongo Fleva imejaa vipaji vingi kutoka kwa wasanii tofauti tofauti, ambao kila mmoja alifanikiwa kutoka kwa wakati wake. Katika hao wapo ambao walianza muziki zamani na wengine hawana muda mrefu kwenye game.Lakini kila mmoja amekuwa na wimbo wake ambao ulimfungulia njia ya mafanikio kwenye muziki.
Nenda Kamwambie ya kwake Diamond Platnumz uliotoka 2009, ukiwa umetayarishwa na Bob Juniour, ulikuwa mwanzo wa mafanikio ya kimuziki kwa msanii huyo.
Wimbo huu ulipokelewa kwa ukubwa kwenye vituo mbalimbali vya habari hasa ikilinganishwa kipindi hicho mitandao ya kijamii ilikuwa haijashika kasi kama ilivyo sasa.
Nenda Kamwambie ulimfanya Diamond kukubalika kwa mashabiki kutokana na uwezo wake wa sauti melodi na uandishi wa kitofauti kitu ambacho wadau wengi wa muziki kipindi hicho waligundua kuwa Mondi ni nyota ajae.
Cinderella ya kwake Alikiba iliyotoka 2006, moja kati ngoma maarufu kwenye muziki wa Bongo Fleva ni hii ya mfalme ambayo ilimtambulisha vyema kwenye muziki na kumpa umaarufu.
Wimbo huu pia ndiyo umebeba jina la albamu yake ya kwanza ya Alikiba iliyotoka 2006 inayofahamika kama Cinderella ambayo ilikuwa na jumla ya nyimbo 15 zikiwemo Macmuga, Naksh Naksh, Njiwa, Raggatone, Kufosi mapenzi, Zaidi Yangu na nyinginezo
Ngoma hii pia ilifanya vizuri kwenye vyombo vya habari huku ikileta mapinduzi makubwa na uhamasisho kwa vijana wengi kuanza kupenda na kufanya muziki wa aina hiyo.
Ubora wa sauti nzuri ya Alikiba uliwachanganya mashabiki wengi na kuanza kumfuatilia mpaka sasa tunaona mafanikio makubwa alioyapata.
Dar Kugumu ya kwake Marioo iliyotoka mwaka 2018, ambayo ilitayarishwa na mikono ya Abba chini ya studio za Abba Music ikiwa ni miongoni mwa nyimbo zilizobeba histori kubwa ya msanii Marioo.
Haikuwa ngoma yake ya kwanza alikuwa tayari ametoa ngoma nyuma lakini hii ilipenya zaidi na kufungua milango lakini pia ilitengeza shauku kwa mashabiki kutaka kumjua Marioo zaidi
Nai Nai ya Ommy Dimpoz akimshirikisha Alikiba, ikiwa moja kati ya ngoma iliosumbua sana mwanzoni mwa mwaka 2010 huku ikitazamwa kama ni miongoni mwa miunganiko bora ya wanamuziki Afrika Mashariki, Alikiba akiwa kama nyota wa mchezo kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa kipindi hicho alifanya makubwa sana na kuibeba ngoma hiyo licha ya kushirikishwa na kuimba kwenye korasi pekee.
Imemtambulisha vyema Dimpoz kwenye gemu ya muziki wa Bongo Fleva huku akiondoka na kijiji cha mashabiki kwenye baadhi ya shoo ambazo amekuwa akifanya tangu wimbo huo kuachiwa rasmi.
Naenda kusema ya kwake Aslay, akiwa kama moja ya vijana walionza muziki wakiwa na umri mdogo ila akaonesha kipaji na uwezo mkubwa kwenye muziki, Naenda Kusema ni miongoni mwa nyimbo kubwa Bongo ambayo ilimleta mjini Aslay na watu wakaamini kwenye kipaji chake licha ya kuwa na umri mdogo aliweza kuonesha kujiamini kwa hali ya juu na utunzi ulio bora zaidi.
Leave a Reply