Ndoa za utotoni zaongezeka Ethiopia

Ndoa za utotoni zaongezeka Ethiopia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto UNICEF, limefahamisha kuwa ndoa za utotoni na unyanyasaji wa kijinsia umeongezeka nchini Ethiopia.

Madaktari na wafanyakazi wa umma wamebaini kuwa kukithiri kwa hali hiyo ni kutokana na ukame unaosababisha njaa na kuzidi kwa umasikini miongoni mwa raia.

Kwa familia nyingi zilizokata tamaa, kumuoza binti yao ni sawa na kupunguza gharama na mahari inayotolewa husaidia katika matumizi mbalimbali.

Aidha shirika hilo linasema ndoa za utotoni, ambazo ni kinyume cha sheria nchini humo zimeongezeka maradufu katika maeneo manne yaliyoathirika zaidi na ukame katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka uliopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags