Ndoa ya Rambo kuvunjika

Ndoa ya Rambo kuvunjika

Moja kati ya taarifa kubwa iliyozua gumza kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusiana na Muigizaji Mkongwe wa Filamu Sylvester Stallone maarufu Rambo  na mkewe wanadaiwa kuachana.

Mke wa Rambo  Jennifer Flavin amewasilisha kesi ya talaka baada ya miaka 25 ya ndoa  yao.

Imeelezwa kuwa Moja ya Sababu zinazotajwa kuwa huwenda zikawa ndio chanzo kikubwa cha Ndoa hiyo kuvunjika ni Mkali huyo wa Filamu kutokuweka Wazi baadhi ya Mali ndani ya Ndoa jambo ambalo  limesababisha hali ya Kiuchumi kuwa mbaya katika Familia yao.

Hata hivyo Baadhi ya Mashabiki walianza kuhisi kutokuwa na Maelewano mazuri katika Ndoa hiyo baada ya Staa huyo wa Filamu Duniani Kuchora mchoro mwingine wa picha ya Mbwa wake Mpya juu ya Picha ya Mke wake aliokuwa Ameichora katika Mkono wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags