Nchi 50 za Magharibi zimehimiza China kuwaachia huru wafungwa wa jamii ya Waighur na kutekeleza kikamilifu mapendekezo yote katika ripoti ya Umoja wa Mataifa inayoituhumu kwa uwezekano wa kufanya uhalifu dhidi ya ubinadamu dhidi ya watu wa jamii hiyo na makundi mengine ya Waislamu.
Nchi hizo zimeitaka China ichukue hatua za haraka kuwaachia huru wale wote wanaonyimwa uhuru wao katika mkoa wa magharibi wa Xinjiang.
Balozi wa Canada katika Umoja wa Mataifa Bob Rae alisoma taarifa katika mkutano wa kamati inayoshughulikia masuala ya haki za binadamu ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa akielezea wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kibinadamu nchini China na kushindwa kwa serikali ya mjini Beijing kujadili matokeo ya ripoti hiyo kuhusu ukiukwaji wa haki za Waighur na makundi mengine ya Waislamu.
Leave a Reply