Nandy asimulia safari yake ya muziki, Amtaja Zuchu

Nandy asimulia safari yake ya muziki, Amtaja Zuchu

Mwanamuziki wa #BongoFleva #Nandy, amesimulia harakati zake za kupambania ndoto zake za kuwa msanii maarufu huku akidai kuwa kuna msanii kutoka kundi la THT alikuwa akimbania.

Nandy ameyasema hayo katika video aliyoi-share kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kueleza kuwa wakati alipokuwa akipambana kujiunga na kikundi cha muziki cha THT kuna msanii alitaka kumbania ili asipewe nafasi kwa kuuliza kama anajua kuimba huku baadhi yao wakidai alikuwa na sauti ya kitoto.

Hata hivyo msanii huyo alifunguka mara ya kwanza kukutana na mwanamuziki Zuchu nchini Nigeria ambapo alieleza kuwa kuna msanii mwenziye ambaye naye alikuwa katika kikundi hicho aitwaye Cris alimshawishi aende Nigeria katika mashindano ya muziki ndipo akakutana na mkali huyo wa ngoma ya ‘Siji’.

Mbali na hayo Nandy alieleza kuwa safari yake ya kwenda Nigeria kupambania ndoto yake ya muziki ilifanikiwa lakini ilikuwa na changamoto baada ya kipindi hicho kuwa na mtihani wa kuhitimu elimu yake ya chuo kikuu ngazi ya Diploma.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags