Nandy akanusha kuwa na Supermarket

Nandy akanusha kuwa na Supermarket

Mwanamuziki, The African Princess, Nandy amlilia Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye baada ya watu wasio waaminifu kutumia jina lake kutapeli umma.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mwanamuziki huyo ameandika kuwa “Ndugu zangu hizo form ukiziona ona kama umeona ukoma, mimi sina supermaket popote na wala sina mpango wa kuwa nayo, mnalipishwa form za kazi mshaona wapi jamani?”.

“Na kuwataka watu kuwa makini kwani hana uhusiano wowote na watu wa supermarket hiyo ambayo inatumia jina lake, jamaani mnaibiwaaaa nisaidieni kusambaza huu ujumbe, haipiti siku sipati malalamiko watu wana ibiwa hii imezidi mno”.“Watu wanatoa mitaji yao, ada zao sababu ya hawa watu! Sikatai mko katika kujitafuta lakini angalau ulizaa mara mbili mara tatu! Au njoo kwa page yangu angalia nishwahi sema nina supermarket?, Poleni wote mliopatwa na hawa watu siku yao yaja” ameandika Nandy

Aidha mwanamuziki huyo alimuomba waziri ili aweze kukomesha tabia hii na kueleza kuwa “Mhe. Nape Nnauye  naomba nisaidie baba naomba niwe mfano kwa hawa wanao tumia jina langu kuumiza watu niko tayari kutoa ushirikiano 100%” ameongea mwanadada huyo anaetamba na kibao chake cha Falling


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post