Nandy afunguka mazito

Nandy afunguka mazito

Ikiwa leo ni jumatatu ya kwanza ya mwaka mpya wa 2022, basi katika gumzo mitandaoni huko tumekusogezea mambo mazito aliyoyasema msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nandy ameandika mazito kwenda kwa mashabiki zake akionesha kuwashukuru na kutaja mipango yake ya mwaka huu mpya.

Mwanadada huyo ambaye anaendelea kujizolea umaarufu kutokana na nyimbo zake amesema 2021 ulikuwa mwaka wa Baraka kwake na kusisitiza kuwa ni miaka sita sasa mashabiki wake wamekuwa naye bila kumchoka hivyo anaingia mwaka mwingine asabi kwa kishindo.

“Bila Mungu, bila nguvu zenu isingewezekana! Tumefanya mengi matukio makubwa ambayo hata mimi nikikaa mwenyewe nawaza nimevukaje hapa! Ila kwa support yenu tumeweza, 2022 najua kila mtu ana wish uwe mwaka mzuri ila pia tusisahau sisi tunapanga na Mungu naye anapanga na maadui nao wanapanga.

“Kikubwa dua Mungu atasimama kama alivyosimama mwaka 2021! Niombe radhi kwa yoyote niliye mkwaza mwaka huu (jana) na me nimewasamehe wote kwani wenye moyo safi huishi kwa Amani,” ameandika Nandy na kuongeza

“Asante kwa kunifanya mwanamke wa mfano role model wa wengi niahidi hii nguvu yam waka huu ni juu yenu 2022 tunayo mengi, In God We Trust,” amesema

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags