Namungo, Fountain Gate wapigwa kalenda Ligi Kuu

Namungo, Fountain Gate wapigwa kalenda Ligi Kuu

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuahirisha mchezo wa ligi baina ya Namungo FC na Fountain Gate FC uliokuwa uchezwe leo katika Uwanja wa Majaliwa Lindi.

Taarifa iliyotolewa na TPLB leo, imesema kuwa tarehe mpya ya kuchezwa mechi hiyo itapangwa.

"Mchezo kati ya @namungofc na @fountaingate_fc umeahirishwa na utapangiwa tarehe nyingine," iliandika TPLB katika ukurasa wake wa Instagram.

Muda mfupi baada ya taarifa hiyo ya TPLB, Namungo FC ambayo ni mwenyeji wa mchezo huo nayo ilithibitisha kutofanyika kwake kupitia ukurasa wake wa Instagram.

"Mchezo wetu wa leo wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate FC ulikuwa ufanyike leo kwenye Uwnaja wa Majaliwa umeahirishwa mpaka utakapopangiwa tarehe nyingine," ilisema taarifa hiyo ya Namungo.

Mwananchi Digital inafahamu kwamba kuahirishwa kwa mchezo huo kumetokana na kundi kubwa la wachezaji wa Fountain Gate kutosajiliwa katika mfumo wa usajili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na lile la soka duniani (Fifa).

Kutosajiliwa huko kumetokana na Fifa kutopata uthibitisho wa Fountain Gate kulipa malipo ya mmoja wa wachezaji wake wa zamani ambaye aliishtaki timu hiyo akidai fidia ya kuvunjiwa mkataba kiholela miaka miwili iliyopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags