Nahreel akanusha kuwa na mtoto wa nje

Nahreel akanusha kuwa na mtoto wa nje

Mtayarishaji wa muziki, Nahreel amekanusha kuwa na mtoto nje huku akifafanua kuwa taarifa zinazosambazwa mtandaoni kuwa amezaa na mwanamke mwingine ni za uongo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nahreel ameeleza kuwa taarifa hizo si za kweli kwani yeye amezaa na mwanamke mmoja tu ambaye ni Aika.

“Kutokana na habari zinazosambaa kwenye blog mbali mbali na watu mbali mbali maarufu pia wamekuwa wakipost bila kuwa na ushahidi wowote, hizi habari sio za kweli. Nina watoto wawili @gold_navykenzo na @jamaika_navykenzo

“Na nimezaa na mwanamke mmoja @aikanavykenzo Kuweni makini mnapotoa habari Familia yetu haiendekezi Umbeya ila hii imevuka mipaka.'' ameandika Nahreel.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags