Nadal avunjika mbavu

Nadal avunjika mbavu

Bingwa wa michuano ya wazi ya tennis ya Australia Rafael Nadal atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki 4 mpaka 6 kutokana na majeruhi ya mbavu aliyoyapata kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Indiani Wells.

Pia imedaiwa kuwa mchezaji huyo huwenda akakosa michuano ya wazi ya Ufaransa (French Open).

Nadal raia wa Hispania alionekaa akipata tabu ya kupumua kwenye mchezo wa fainali ya michouano ya Indian Wells siku ya Jumapili mchezo ambao alipoteza kwa kufungwa na Taylor Fritz, na kuna muda wakati wa mchezo huo ilibidi apatiwe matibabu.

Baada ya bingwa huyo mara 21 wa Grand slam kurejea nyumbani kwao nchini Hispania alikutana na Daktari Angel Ruiz-Cotorro kwa ajili ya uchunguzi na imebainika kuwa moja ya mbavu zake imepata ufa hivyo kutokana na tatizo hilo itamchukua wiki 4 mpaka 6 kupona jeraha hilo ili awezekurejea tena kwenye hali ya kucheza tena Tennis.

Kufuatia taarifa hiyo, Nadal ameweka wazi kuwa hizi sio taarifa nzuri kabisa kwake hasa ukizungatia jinsi ambavyo alikuwa ameuanza mwaka huu vizuri.

Kipindi hicho cha wiki 4 mpaka 6 atakachokuwa akitibu majeruhi yake atakosa muda wa kutosha wa kujiandaa na michuano ya wazi ya Ufaransa (French Open) itakayoanza Mei 22, 2022 mpaka Juni 05.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags