Nabeel afariki, Chino ahamishiwa Muhimbili

Nabeel afariki, Chino ahamishiwa Muhimbili

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Nabeel ambaye alikuwa dereva kwenye gari lililombeba mwanamuziki na Dancer #ChinoKid pamoja na wenzake, amefariki dunia kufuatia ajali ya gari iliyotokea siku ya jana.

Asubuhi ya leo Mtayarishaji wa muziki #AbbahProcess amethibitisha taarifa hiyo ya masikitiko ambapo amesema wamempoteza mwanafamilia mwenzao ambaye amemtaja kwa jina la Nabeel.

Hata hivyo inaelezwa kuwa Chino amepata majeraha sehemu ya kifua  na sasa yupo hospitali ya Taifa Muhimbili huku baadhi ya ‘madansa’ wake  wanadaiwa kuvunjika miguu.

 Ikumbukwe kuwa ajali hiyo ilitokea jana eneo la Kabuku ambapo gari lao aina ya Alphard iligongana na Lori la mafuta.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags