Mzee wa Buga aingia mitini show Tanzania

Mzee wa Buga aingia mitini show Tanzania

Duuuuuuuuh! Sio powa yani bwana kwa taarifa za kusikitisha yule mzee wa Buga Kizz Daniel usiku wa kuamkia leo alitakiwa kufanya show ambayo ilipewa jina la Summer Applified lakini mambo yakatindinganya hakuweza kufika katika show hiyo.


Pamoja na Kizz Daniel kutua kwenye ardhi ya Tanzania staa huyo hakufanikiwa kufanya show hiyo. Sababu za Kizz Daniel kutotokea Jukwaani hazijafahamika mpaka sasa, Tunajaribu kuwasiliana na uongozi wa waandaji wa show hiyo kujua nini haswa kimepelekea staa huyo anayetamba na wimbo wake buga ambae alimshirikisha msanii mwenzie Tekno

Aidha licha mwamba huyo kutotokea jukwaani mastaa wengine kutokea nchini Tanzania kama Marioo, Salaphina, Mabantu, Younglunya walifanikiwa kufika na kutoa burudani kwa mashabiki kama ilivyo takiwa.

Kupitia show hiyo ambayo imefanika katika ukumbi wa Ware House zamani Nexrdoor ambapo kiingilio kilikuwa ni elfu 80,000 kwa kawaida na VIP ikiwa ni 150,000

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags