Mzaliwa wa kigoma ang’ara Marekani

Mzaliwa wa kigoma ang’ara Marekani

Benard Kamungo mzaliwa wa kasulu, Kigoma anayeichezea ‘klabu’ #FCDallas inayoshiriki ‘ligi’ kuu ya nchini Marekani ameitwa katika kikosi cha awali cha Marekani, chini ya miaka 23 kitakachoshiriki michezo ya Olimpiki mwakani.

Kamungo alihamia Abilene, Texas nchini Marekani mwaka 2016 baada ya familia yake kupata msaada kutoka kwa kamati ya kimataifa ya uokoaji (IRC).

Juni 2023 , aliitwa na ‘timu’ ya Taifa ya Tanzania, lakini hakucheza kufika kwa kile ilichoelezwa kuwa ni changamoto ya passport ya kusafiria.

Akiwa katika mazoezi ya kikosi cha Marekani ambacho kitacheza ‘mechi’ mbili za kirafiki dhidi ya #Japan na #Mexico, Kamungo anatakiwa kuonesha uwezo wa juu ili kupata nafasi katika orodha ya mwisho ya kikosi kitakachoiwakilisha Marekani.
.
.
.
#MwananchiScoop.
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags