Myanmar kuwaachia huru wafungwa 6,000 wakiwemo raia wa kigeni

Myanmar kuwaachia huru wafungwa 6,000 wakiwemo raia wa kigeni

 

Utawala wa kijeshi wa Myanmar umetangaza kuwa leo, utawaachia huru wafungwa wapatao 6,000 akiwemo balozi wa zamani wa Uingereza, mwandishi wa habari wa China na mshauri wa kiuchumi kutoka Australia.

 Afisa mmoja mwandamizi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wote watatu watasafrishwa na kurejeshwa nchini mwao bila ya kutaja tarehe.

Wanawake wapatao 600 ni miongoni mwa wafungwa watakaoachiwa huru katika maadhimisho ya siku ya kitaifa yanayofanyika leo.

 Taifa hilo la kusini mashariki mwa Asia limekuwa katika machafuko tangu yalipofanyika mapinduzi ya kijeshi mwaka jana na kushuhudia ukandamizaji wa umwagaji damu dhidi ya wapinzani ambao umesababisha maelfu ya watu kufungwa jela. Raia kadhaa wa kigeni wamejikuta katika mtafaruku huo.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post