My Darling Yashika Namba Moja Shazam

My Darling Yashika Namba Moja Shazam

Wimbo ‘My Darling’ wa msanii kutoka Nigeria, Chellaboi umeshika nafasi ya kwanza katika mtandao wa ‘Shazam’ na kuingia katika orodha ya ngoma zilizotafutwa zaidi duniani.

My Darling ambao umetoka wiki tatu zilizopita, imefanikiwa kujizolea umaarufu kupitia mitandao ya kijamii kama vile Tiktok, Facebook, na Instagram huku ikishika namba moja kwenye jukwaa la Boomplay.

Hata hivyo msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz alichapisha video ya Chella kupitia ukurasa wake wa Instagram akionekana akiifurahia ngoma hiyo. Huku verse ya Diamond ikisikika kwa mbali na kuthibitisha ujio wa remix ya ngoma hiyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyo kutengeneza ngoma na kupenya zaidi kwenye soko la Kimataifa. Septemba 18, 2024 alifanikiwa kutoa ngoma ya ‘Nyash’ ambayo ilikuwa ya kwanza tangu kuanza kwake muziki.

Chella ambaye ana mwaka mmoja kwenye muziki mbali na kutambulika kupitia ngoma ya Nyash na My Darling lakini pia ana Ep yake ya Tears Of A Mad Man yenye jumla ya nyimbo tano ambazo ni Wahala, Iweriwe Love, Bill, Broke, na Ewo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags