Mwijaku ameyakanyaga kwa Maua Sama

Mwijaku ameyakanyaga kwa Maua Sama


Ikiwa zimepita siku chache tangu muigizaji na mtangazaji Mwijaku kumzungumzia vibaya mwanamuziki Maua Sama mazungumzo ambayo yaliyoonekana ni unyanyasaji, Maua Sama kupitia wakili wake Claudio Msando, wamemuandikia Mwijaku hati ya madai huku ikimpa saa 24 ya kujibu tuhuma hizo za udhalilishaji pamoja na fidia ya tsh 300 milioni.

Kufuatiwa na hati hiyo pia imeeleza kuwa endapo Mwijaku atashindwa kufanya hivyo basi kesi hiyo itapelekwa mahakamani kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.

Ukiachiliambali kuchapishwa kwa hati hiyo, hata hivyo Mwijaku kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya jana alimuomba msamaha mwanamuziki huyo kwa maneno aliyoyazungumza kama yamemuumiza kwa namna yoyote ile kwani yeye alichukulia utani kutokana na wawili hao kuzoea kutaniana.

Ikumbukwe kuwa Mwijaku alizungumza maneno ya udhalilishaji wakati alipokuwa kwenye usiku wa miaka 20 ya King.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags