Mwijaku Akutwa na Kesi ya Kujibu

Mwijaku Akutwa na Kesi ya Kujibu

Ohoo!!Msanii wa maigizo, Burton Mwembe maarufu Mwijaku,wenyewe anapenda kujiita Dc wa Insta amekutwa na kesi ya kujibu katika shtaka la kusambaza picha za utupu kinyume na sheria linalomkabili.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu,Rhoda Ngimilanga ametangaza uamuzi huo baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wa mashahidi watano na vielelezo vinne.

Mwijaku anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019 katika jiji la Dar es salaam.
Msanii huyo anadaiwa kuchapisha picha za ngono kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp uliounganishwa katika kompyuta.

Hata hivyo Mwijaku ataanza kujitetea juu ya kesi hiyo mnamo Mei 10, 2022

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags