Mwigizaji wa nigeria, Amaechi afariki dunia

Mwigizaji wa nigeria, Amaechi afariki dunia

Ikiwa zimepita wiki tatu tangu kitokee kifo cha mwigizaji kutoka Nigeria Mr Ibu, sasa imeripotiwa kifo cha mwigizaji mwingine kutoka nchini humo anayefahamika kwa jina la Amaechi Muonagor (62).

Kwa mujbu wa vyombo vya habari nchini humo vimeeleza kuwa mwigizaji huyo alifariki Jumapili, Machi 24, akiwa kwenye matibabu ya dialysis baada ya figo yake kushindwa kufanya kazi.

Inaelezwa kuwa wiki moja kabla ya kifo chake aliomba masaada kwa ajili ya kupata pesa za matibabu ya upandikizwaji wa figo nchini India. Amaechi aliwahi kuonekana katika filamu ya Aki and Pawpaw’, Meet the in Laws’, ‘Aka Gum’, ‘My Village People’, ‘Isakaba’ ‘the Village boys I love’.

Kutokana na taarifa za kifo hicho watu mbalimbali wameendelea kutoa salamu za pole kupitia mitandao ya kijamii akiwemo Mchambuzi wa Masuala ya Kijamii na Mwenyekiti wa Chama cha Michezo cha Jimbo la Delta, Morris Monye, ameonesha kuumizwa na taafifa za kifo hicho.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X ameandika "Nimehuzunishwa sana na habari za kifo cha Amaechi Muonagor. Alikuwa mwigizaji mahiri wa Nollywood ambaye uwepo wake kwenye skrini zetu ulikuwa mzuri sana". Morries ameandika

Pamoja na hayo Chama cha Waigizaji cha Nigeria, AGN, bado hakijatoa tamko lolote.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags