Mwigizaji O. J. Simpson afariki dunia

Mwigizaji O. J. Simpson afariki dunia

Mwanamichezo wa zamani ambaye pia alikuwa mwigizaji kutoka nchini Marekani Orenthal James Simpson maarufu kama O. J. Simpson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76, baada ya kusumbuliwa na Saratani ya tezi dume iliyogundulika miezi miwili iliyopita.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na familia yake siku ya jana Alhamisi Aprili 11, kupitia ukurasa wake wa X wakieleza kuwa Simpson alifariki Aprili 10, kutokana na ugonjwa wa Saratani huku familia ikiwataka wadau mbalimbali kutoingilia faragha yoyote ili kuweza kumpumzisha ndugu yao kwa Amani.

Simpson aliwahi kufunguliwa mashitaka ya kumuua mkewe wa zamani Nicole Brown huku mwaka 1995 akifutiwa mashitaka hayo, baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Si hayo tuu pia mwaka 2008, alihukumiwa kifungo cha miaka 33 jela kwa kesi ya wizi wa kutumia silaha na kuachiwa huru mwaka 2017.

Orenthal James Simpson alizaliwa jijini San Francisco, California, nchini Marekani na alianza kupata umaarufu wakati akiichezea ‘ligi’ kuu ya NFL ( American Football).

Amewahi kuonekana katika filamu mbalimbali za ngumi pamoja na drama zikiwemo ‘The Naked Gun: From the Files of Police Squad’, ‘The Murder of Nicole Brown Simpson’, ‘The O. J. Simpson Story’, ‘The Towering Inferno’, ‘Cocaine and Blue Eyes’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags