Mwigizaji Junior Pope kuzikwa leo

Mwigizaji Junior Pope kuzikwa leo

Mwili wa marehemu mwigizaji kutoka nchini Nigeria Pope Odonwodo umewasili katika kijiji alichozaliwa cha Ukehe Igbo-titi Local Government Area Jimbo la Enugu, kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vimeripoti kuwa Pope atazikwa siku ya leo Mei, 17, 2024 baada ya misa kukamilika ambayo inafanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro huko Ukehe.

Pope Odonwodo alifariki April 10, 2024 pamoja na watu wengine baada ya boti walilopanda kupinduka katika Mto #Anam, ambapo imeripotiwa kuwa Pope alipanda kwenye boti hiyo kwa ajili ya matayarisho ya filamu yake mpya.

Marehemu #Pope ameacha mke na watoto watatu, amewahi kuonekana katika filamu mbalimbali zikiwemo ‘Okija & Pamela’, ‘Honey Money’, ‘No Way Through’, ‘Wrong Initiation’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags