Wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikielekeza bondia Hassan Mwakinyo kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazeti la Mwananchi kufuatia kesi ya madai inayomkabili, wakili kiongozi wa kampuni ya uwakili ya Haki Kwanza, Alloyce Komba amebainisha mambo yanayoweza kumkabili kama ataendelea kutotokea.
Juzi, kesi hiyo ilitajwa kwa mara ya kwanza na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Amiri Msumi aliyetoa uamuzi wa bondia huyo kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazeti baada ya Mwakinyo kukataa kupokea hati ya wito iliyowasilishwa kwake na msambaza nyaraka wa Mahakama.
Akizungumza kwa muktadha wa kisheria, Komba amesema “Kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazeti ni samansi mbadala. Kama Mwakinyo atakwenda mahakamani Novemba 20, 2023 ili kusikiliza kesi yake itakapotajwa tena, basi itasikilizwa pande zote mbili na kujitetea.
“La sivyo upande wa mdai ukiomba isikilizwe upande mmoja ikileta ushaidi wake (ex parte hearing) ikaamuriwa hivyo, Mwakinyo hatatafutwa tena matokeo yake ni asubiri hukumu ya upande mmoja (ex parte judgment) ambayo huwa na madhara makubwa.
“Mdai akishinda atapata decree (ya kukazia hukumu) anaweza kukamata akaunti za benki au mali zake mdaiwa,” amesema.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply