Mwanamuziki Megan Thee Stallion ashtakiwa

Mwanamuziki Megan Thee Stallion ashtakiwa

Label ya 1501 Certified Entertainment iliyokuwa ikimsimamia Mwanamuziki Megan imemshtaki msanii huyo kwa kuachana nayo kwa ugomvi.

Kutokana na madai hayo, label hiyo imeamua kumshtaki ikidai kwamba albamu ya Megan ya mwisho haikuwa nzuri wala mauzo yake hayakuwa makubwa kama vile wanavyotaka na bado wanamdai kazi nyingi pamoja na kiasi kikubwa cha fedha.

Kwa mujibu wa tweet ya msanii huyo katika ukurasa wake wa Twitter ilieleza kuwa anashtakiwa na label hiyo.

“Kwanza kabisa jamaa kutoka label yangu alisema kwamba simtengenezei fedha ya kutosha na sasa ananishtaki ili niendelee kuwa kwenye label yake kwa sababu tu anataka niendelee kumwingizia pesa zaidi lol…. Sasa kama sikuingizii pesa nyingi kwa nini usiachane na mimi,” aliandika Megan






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags