Mwanamke wa kwanza kutawazwa kuwa mchungaji

Mwanamke wa kwanza kutawazwa kuwa mchungaji

Katika maeneo mengi ya kikristo duniani, kuwa na viongozi wa kike wa kanisani si jambo geni sana. Lakini mpaka sasa, nchi takatifu ambapo matukio mengi katika biblia yamewekwa  ilikuwa haijawahi kutokea mwanamke kutoka ndani ya nchi hiyo kuwa kiongozi wa dini.

Siku ya Jumapili, ilikuwa sherehe ya raia wa Palestina kutoka Jerusalem, Sally Azar, kuwa mchungaji mwanamke wa kwanza katika kanisa la Kilutheri katikati ya mji mkongwe, iliyohudhuriwa na mamia ya watu kutoka mataifa mbalimbali.

"Nilifurahishwa zaidi kuona msisimko wa watu wengine." Mchungaji ni hisia isiyoelezeka kuchukua hatua hii kwa kuungwa mkono na kanisa." alisema Sally.

"Nina matumaini kwamba wasichana na wanawake wengi watajua kuwa jambo hili linawezekana na hata wanawake wengine kutoka kwenye makanisa mengine watajiunga nasi. Najua itachukua muda mrefu, lakini nadhani itafurahisha zaidi ikiwa hii hali itabadilika nchini Palestina,” amesema.

Aidha Wakristo ni wachache katika maeneo ya Palestina, Israel na Jordan. Wakristo wengi hapa ni wa Kanisa la Orthodox la Ugiriki na kuna makanisa ya kikatoliki ya Latini, ambayo hayaruhusu mapadre wanawake.

Idadi ya wanawake wanaowekwa wakfu katika makanisa ya Kiprotestanti inaongezeka katika miongo michache iliyopita. Na hii inawapa fursa ya kuwa viongozi wa shule na hospitali katika ardhi takatifu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post