Mwanamke adaiwa kufariki baada ya kula dagaa

Mwanamke adaiwa kufariki baada ya kula dagaa

Mwanamke mmoja adaiwa kufariki dunia na watu wengine 12 wamelazwa kwa matibabu baada ya kula dagaa wenye sumu katika Mgahawa mmoja huko nchini Ufaransa eneo la Bordeaux.

Aidha shirika la Afya la Ufaransa limesema kuwa dagaa hao walihifadhiwa nyumbani kwa mmiliki wa mgahawa huo nakupelekea  kuzuka kwa ugonjwa utokanao na chakula Bordeaux, unaosadikiwa kusababishwa na dagaa hao.

Hata hivyo inadaiwa wagonjwa wengi waliyolazwa ni raia wa Uingereza na Ireland ambao wapo nchini Ufaransa kwa mapumziko (vacation).

Mashirika ya Afya ya Uingereza na Ufaransa wamehimiza raia wake waliyopo maeneo hayo na waliokula katika mgahawa huo hivi karibuni kuwahi hospitali kwa vipimo na matibabu. Kwani ugonjwa huo ni hatari na husababishwa na sumu inayotokana na bakteria ikiwa chakula hakikuhifadhiwa vizuri.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags