Mwanamitindo kutoka Uingereza, Naomi Campbell amepigwa marufuku kuwa mdhamini mkuu wa Shirika la misaada la ‘Fashion For Releaf’ baada ya kugundulika kuwa amekuwa akitumia pesa za misaada katika matumizi yake binafsi.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vinaeleza kuwa sakata hilo limegundulika katika kipindi cha miaka mitano ambapo shirika analolisimamia lilichangisha zaidi ya Sh 17 bilioni lakini lilitoa Sh 1 bilioni tu katika mashirika yanayohudumia watu wenye uhitaji.
Uchunguzi umebaini kuwa Campbell alikua akitumia pesa nyingi za Shirika hilo katika matumizi yake binafsi ikiwemo kuishi katika Hoteli za gharama, matibabu ya mwili na kulipa walinzi wake.
Campbell amefungiwa kushiriki kusaidia sehemu yoyote ile huku akiondolewa mazima kwenye shirika ‘Fashion For Relief’ alilolianzisha mwaka 2005 kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Aidha tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo ilipeleka mipango ya miradi ya mitindo katika mataifa mbalimbali likiwemo Tanzania, New York, London, Cannes, Moscow na Mumbai.
Leave a Reply